Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati mkutano wa baraza la uchumi na jamii ukianza wanawake ndio ajenda kuu

Wakati mkutano wa baraza la uchumi na jamii ukianza wanawake ndio ajenda kuu

Mkutano wa ngazi ya juu wa kitengo cha baraza la uchumi na jamii ECOSOC umeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York.

Mkutano huo utakaomalizika Julai pili unajadili masuala ya usawa wa kijinsia, kumuwezesha mwanamke, mtazamo wa usawa wa kijinsia katika malengo ya maendeleo ya milenia na changamoto za ushirikiano wa kimataifa wa maendeleo. Rais wa ECOSOC raia wa Malaysia Hamidon Ali katika taarifa yake ya ufunguzi amesema licha ya kwamba watu wengi hivi sasa wamelelimishwa lakini bado wanawake na wasichana wanakabiliwa na ubaguzi wa kijinsia.

Ameongeza kuwa wakati lengo la tatu la maendeleo ya milenia linashabihiana moja kwa moja na kuwapa uwezo wanawake, malengo mingine yote yanategemea wanawake kuwa na kauli katika maendeleo yao. Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesisitiza umuhimu wa usawa wa kijinsia na malengo ya milenia.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)