Wacheza kandanda mashuhuri watoa wito wa kuufunga bao umasikini

14 Juni 2010

Wakati michuano ya kombe la dunia inaendelea nchini Afrika ya Kusini mabalozi wema wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP, Didier Drogba na Zinedine Zidane, wamezindua tangazo la televisheni la kupiga vita umasikini.

Tanzazo hilo linaitaka dunia kuwa tayari kwa changamoto na kujiunga na timu itakayo ushinda umasikini. Drogba ambaye ni mchezaji wa timu ya Uingereza ya Chelsea na kampeni wa timu ya Taifa ya Ivory Coast amesema hakuna watazamaji katika vita dhidi ya umasikini wote tunahitajika uwanjani ili kuboresha maisha ya mamilioni ya watu masikini duniani.

Tangazo hilo kwa ajili ya jamii lililorekodiwa kwa lugha mbalimbali litakuwa likitangazwa na kuonyeshwa wakati wote wa mashindano ya kombe la dunia Afrika Kusini na lengo likiwa ni kutia motosha juhudi za kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ambayo ni manane na yaliafikiwa na kukubalika kimataifa ambayo ni pamoja na kupunguza umasikini, njaa, vifo vya watoto na kina mama wajawazito,magonjwa, malazi na usawa wa kijinsia ifikpo mwaka 2015.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter