Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imeelezea wasiwasi kuhusu kuchelewa shughuli za uokozi Malta

UNHCR imeelezea wasiwasi kuhusu kuchelewa shughuli za uokozi Malta

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia Wakimbizi, UNCHR limeelezea wasi wasiwake kuhusiana na kuchelewa kwa juhudi za kuitafuta na kuiokoa meli inayobeba zaidi ya watu 20 karibu na Malta wengi wao wakiwa ni kutoka Eretrea.

Meli hiyo ambayo abiria wake ilikuwa pamoja na wanawake watatu na mtoto wa miaka nane hatimaye imeokolewa na meli ya Libya hapo jana.