Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Libya yataka shirika la UNHCR kufunga ofisi zake na kuondoka nchini humo

Libya yataka shirika la UNHCR kufunga ofisi zake na kuondoka nchini humo

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia Wakimbizi, UNHCR, limepokea amri kutoka kwa serikali ya Libya kusitisha shughuli zake na kufunga ofisi zake za nchini humo.

UNHCR imesema imesikitishwa na hatua hiyo kwani wataoathirika zaidi na maelfu ya watu wanaohitaji msaada wa shirika hilo.

Shirika la UNHCR limekuwa likifanya kazi nchini Libya kuwalinda, kuwasaidia na kutafuta suluhisho la kudumu kwa wakimbizi na watu wanaotafuta hifadhi walioko nchini humo.

Wakati huo huo, UNHCR inajaribu kushauriana na serikali ya Libya ili isalie nchini humo na inamatumaini kuwa suluhu itapatikana. Wengi wa wakimbizi walioko Libya ni kutoka Eritrea, Ethiopia na mashariki ya Kati.