Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

SONY, FIFA na UNDP kuwaonyesha wacameroon kombe la dunia bure kuchagiz malengo la milenia

SONY, FIFA na UNDP kuwaonyesha wacameroon kombe la dunia bure kuchagiz malengo la milenia

Wakati wa Kombe la dunia nchini Afrika ya Kusini likijongea ,Shirikisho la Kandanda duniani, FIFA , kampuni ya kutengeneza vifaa vya umeme Sony na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP wamezindua kampeni ya kuhakikisha malengo manane ya Milenia yanafikiwa itakapotimu mwaka 2015.

Kampeni hiyo iliyozinduliwa nchini Cameroun itaangazia lengo la Sita la kupambana na Ukimwi katika maeneo ambayo kuna maambukizi ya hali ya juu.

Sony na UNDP wataweka televisheni kubwa ilikuonyesha mechi nane za Kombe la dunia katika maeneo tofauti na kuwasaaidi watu kutazama mechi hizo katika maeneo ya Bamende, tarehe 14-15 mwezi Juni, Nkongsamba tarehe 17 mwezi wa Juni, Buea tarehe 19 Juni na Mbalmoyo tarehe 23-24 June bila malipo wakati timu ya Cameroun ikicheza na timu zingine.