Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kulinda haki za wahamiaji kwani wanamchango

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kulinda haki za wahamiaji kwani wanamchango

Kuwaacha wahamiaji bila ulinzi na bila kujua wafanyalo kutaathiri manufaa ambayo yangepatikana kwa mataifa wanakotoka na mataifa wanayoelekea.

Mkutano wa shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo UNDP umekubaliana kuwa serikali zinahitaji kutambua mchango wa wahamiaji kwa maendeleo ya kiuchumi kwa mataifa wanakotoka na mataifa wanamoishi.

Mkutano huo umetoa wito wa kuboreshwa kwa hali ya wahamiaji na kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya usafiri wa wanadamu