Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya kimataifa ya muingiliano wa mila na utamaduni

Leo ni siku ya kimataifa ya muingiliano wa mila na utamaduni

Wataalamu huru wa siku ya kimataifa ya tofauti ya mila kwa ajili ya maendeleo na maridhiano wamesema tofauti za mila zinaweza kunawiri katika mazingira ambayo yanalinda misingi ya uhuru na haki za binadamu.

Wataalamu hao wanasisitiza kuwa kulinda tofauti za mila kunakwenda sanjari na kuheshimu utu wa mtu bila kujali anakubatia utamaduni gani.

Katika taarifa ya pamoja kundi hilo la wataalamu limesema kuwa tofauti za kimila zinaweza kulindwa na kukuzwa iwapo haki za binadamu na misingi ya uhuru, kama uhuru wa kujieleza, uhuru wa habari na mawasiliano, uhuru wa kutobaguliwa kwa njia yeyote sambamba na mtu kuwa na uwezo wa kuchagua kujieleza kimila na kuwa na haki ya kushiriki au kutoshiriki katika mila ya jamii fulani.