Skip to main content

Bara la Afrika lahitaji mshikamano ili kujikomboa:Asha Rose Migiro

Bara la Afrika lahitaji mshikamano ili kujikomboa:Asha Rose Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi Asha Rose Migiro amesema kuwa mshikamano ni muhimu kuwepo kwa mataifa ya Afrika.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa siku mbili jana jioni mjini Bologna nchini Italy Asha Rose Amesema mataifa mengi ya Afrika yamechukua hatua za kijasiri kujenga maisha bora ya siku za usoni kwa raia wake.

Amesema kwa sababu hiyo kwa mara ya kwanza nchi nyingi za afrika zimeweza kuwa na ukuaji wa uchumi wa asilimia tano kwa muda wa miaka kadhaa licha ya uchumi wa dunia kudorora hivi karibuni. Ameongeza kuwa mataifa ya Afrika yamekuwa msitari wa mbele kukiri kuwa katika enzi hii ya utandawazi juhudi za taifa moja pekee haziwezi kuleta ufanisi mkubwa.