Mkutano wa elimu kwa mtoto wa kike umemalizika Dakar Senegal

Mkutano wa elimu kwa mtoto wa kike umemalizika Dakar Senegal

Mkutano wa kimataifa kuhusu elimu kwa mtoto wa kike umemalizika leo mjini Dakar nchini Senegal.

Mkutano huo uliwaleta pamoja viongozi kutoka nchi mbalimbali, wadau wa elimu, mashirika yasiyo ya kiserikali, wanaharakati wa haki za watoto wa kike na Umoja wa Mataifa.

Mada ambazo zimechambuliwa kuhusu elimu ni pamoja na haki ya mtoto wa kike kusoma, kupinga ukatili dhidi ya mtoto wa kike, fursa ya kusoma na ubora wa elimu.