Mapambana ya ukatili wa kimapenzi yaongezwe:Wallstrom
Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kimapenzi Margot Wallstrom amekuwa na mkutano na wajumbe wa tume ya Ulaya kuhusu ukatili huo mjini Brussels.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao chao Bi Wallstrom ameutaka muungano wa Ulaya kujihusisha zaidi katika kukabiliana na ukatili wa kimapenzi wakati na baada ya migogoro ya kutumia silaha .
Amesema labda muungano huo kupitia uteuzi kuhakikisha kwamba azimio la baraza la usalama linatekelezwa kama sehemu ya sera ya Ulaya ya ulinzi na usalama. Kwa upande wake amewataka kuhakikisha ulinzi wa wanawake unapewa kipaumbele na ukatili wa kimapenzi uchukuliwe kama tishio la usalama.