Lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuhakikisha usalama:Ban
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ripoti yake kwenye mkutano wa umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo ya usalama wa watu tangu mkutano wa kimataifa wa 2005 amesema ili kuhakikisha usalama wa watu wito unatolewa kwa wahusika, kuchukua hatua madhubuti na za kuzuia madhara.
Ameongeza kuwa kuna ongezeko la kutegemeana baiana ya hatari inayowakabili watu na jamii zao. Ameongeza kuwa mtazamo huo utasaidia kutoa kipaumbele kwa vitisho vilivyopo sasa, kujua chanzo chake na kusaidia kuchukua tahadhari za awali kuepuka madhara yanayoweza kutokea.
Ripoti yake pia imetaja kuwa kwa pamoja malengo haya ya kuishi bila woga, kuwa huru na haki ya kuishi kwa wote itawezekana.