Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udhibiti wa taka za chuma utasaidia katika maendeleo endelevu:UNEP

Udhibiti wa taka za chuma utasaidia katika maendeleo endelevu:UNEP

Ili kuwa na uchumi wa kimataifa unaozingatia maadili ya mazingira, technilojia safi ya kuzalisha umeme na nishati vitategemea kwa kiasi kikubwa urahisi wa kubadilishwa kwa takataka au mabaki ya chuma na kugeuzwa kuwa vitu vya manufaa.

Vyuma hivyo vinahitajika kwa ajili ya kutengeneza mvuke wa upepo wa kuzalisha umeme wa sehemu ya magari ya kisasa na taa za umeme ambazo hutumia nishati safi isiyo na athari kwa mazingira.

Japo nishati hiyo inaweza kupatikana kiasili lakini inapatikana kwa kiasi kidogo mno na katika maeneo machahe duniani.

Licha ya bei zao kuwa ghali na pia kuwa adimu, ni karibu asili mia moja ya takaka taka za vyuma hivyo zimeweza kubadilishwa na kuwa vitu vya manufaa, huku zingine zikitupwa baada ya kutumiwa. Taarifa hii ni kwa mujibu wa ripoti ya awali ya shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira (UNEP).