Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wajiandaa na kongamano wiki ijayo Uturuki kwa ajili ya kuisaidia Somalia

UM wajiandaa na kongamano wiki ijayo Uturuki kwa ajili ya kuisaidia Somalia

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Ahmedou Ould-Abdallah, amesema wakati wa kuchukua hatua kuinusuru Somalia ni sasa.

Abdallah ameyasema hayo kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo. Na ameongeza kuwa kwamba mkutano wa wiki ijayo mjini Istanbul Uturuki wa msaada kwa Somalia ni kutafuta suluhu mbadala tofauti mambo yaliyozoeleka au kujiondoa nchini humo.

Amesema kila siku amekuwa akisistiza kuwa mchakato wa amani ya Somalia una mambo matatu yanayoingiliana nayo ni maridhiano, usalama na maendeo. Amesema mambo hayo matatu lazima yashughulikiwe kwa pamoja . Bwana Ould-Abhallah ameongeza kuwa mkutano wa Istanbul unaofadhiliwa kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa na serikali ya Uturuki , unatoa fursa muhimu kuisaidia jamii ya wafanya biashara kufanya kazi za kuindeleza jamii ya Somalia.

Mwakilishi huyo pia amesema hali mbaya nchini Somalia lazima ishughulikiwe sambamba na kuwachukulia hatua wanaokiuka haki za binadamu ambao wanachangia machafuko kuendelea.

Kuhusu suala la kukabiliana na tatizo la maharamia linaloongezeka katika pwani ya Abdallah amependekeza nchini zinazovua katika eneo hilo ziwe na akaunti maalumu ya kuweka fedha zinakazopelekwa moja kwa moja serikali ya Somalia kuliko kuwalipa mawakala binafsi ambao huenda wakazitumia fedha hizo kwa mambo mengine.