Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano unahitajika kuhakikisha maisha endelevu asema afisa wa UM

Ushirikiano unahitajika kuhakikisha maisha endelevu asema afisa wa UM

Kikao cha tume ya maendeleo endelevu kimeanza kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa mjini New York.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa na nchi wanachama wanaohudhuria kikao hicho cha 18 cha tume ya maendeleo endelevu wamesema kuna haja ya haraka ya kutimiza ahadi za kulinza maliasili za dunia ili kuhakikisha maisha bora kwa wote.

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi Jomo Kwame Sundaram amesema kwamba kwa kuzingatia uharibifu unaofanywa na binadamu kwa viumbe vilivyo katika hatari ya kutoweka, mmomonyoko wa udongo, ukataji miti na kupungua kwa samaki, ni dhahiri kwamba dunia inalemewa katika Nyanja mbalimbali.