Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa Bon umeweka mikakati kupunguza kiwango cha joto

Mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa Bon umeweka mikakati kupunguza kiwango cha joto

Mkutano wa ngazi ya juu wa mabadiliko ya hali ya hewa unaofanyika Bon Ujerumani na kushirikisha mataifa 45, umepiga hatua katika njia za kupunguza ongezeko la joto duniani.

Hata hivyo kwa mujibu wa waziri wa mazingira wa Ujerumani katika mkutano huo bado maswala mengine nyeti hayajapata ufumbuzi. Wajumbe katika mkutano huo ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa wamekiri kuwa mkutano huo ni hatua muhimu ambayo itachangia katika kupatikana kwa suluhu ya matatizo ya hali ya hewa.

Baadhi ya mafanikio ya mkutano huo ni pamoja na kuafikiana kulinda misitu na ubadilishanaji wa tekinolojia ya hali ya hewa, kutoka kwa mataifa tajiri kwenda kwa mataifa masikini.

Lakini katika kupunguza kiwango cha gesi inayoharibu hali ya hewa, ruzuku kwa nchi masikini na jinsi ya kutathimini kiwango cha pesa na gesi ni masuala ambayo hayajapata ufumbuzi.