Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukaji wa haki za binadamu unachangia umasikini mkubwa Afganistan

Ukiukaji wa haki za binadamu unachangia umasikini mkubwa Afganistan

Ripoti ya ofisi ya kamishna mkuu wa tume ya haki za binadamu iliyochapishwa leo inasema ukiukaji wa haki za binadamu unaongeza ufukara nchini Afghanistan.

Inasema vitendo vya ukandamizaji, ufisadi, uvunjaji sheria, na kuzingatia mipango ya muda mfupi ya matatizo ya usalama kuliko kuangalia mipango ya muda mrefu inayoleta maendeleo, kumechangia ongezeko la umasikini kwa watu zaidi ya theluthi mbili nchini humo ambao tangu hapo ni masikini.

Ripoti hiyo inaongesha kiwango cha kutisha cha watu walioko katika umasikini miaka minane baada ya mkataba wa Bonn ulioahidi mwanzo mpya miongo kadhaa baada ya vita.

Licha ya msaada wa dola bulioni 35 katika mwaka 2002 hadi 2009 asilimia 36 ya Waafughanistan wanaaminika kuishi katika umasikini. uliokithiri.