Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zinazochafua zaidi mazingira ziko tayari kuwajibika

Nchi zinazochafua zaidi mazingira ziko tayari kuwajibika

Nchi ambazo zinahusika na uchafuzi wa mazingira kutokana na gesi ya viwandani kwa zaidi ya robo, sasa zimeamua kuunga mkono mkataba ulioafikiwa kwenye mkutano wa mwaka jana Copenhagen Denmark.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema hatua hiyo ni muhimu saana katika kuelekea mkutano ujao wa hali ya hewa. Mkutano ujao unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba mjini Cancun Mexico, ukiwa na lengo la kuwa na mkataba wa kisheria wa kimataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa.

Katika maandalizi ya mkutano ujao bwana Ban anasema Umoja wa mataifa unashirikiana kwa karibu na serikali ya Mexico. Lakini amesema kwa sasa ametiwa moyo na hatua iliyofikiwa.