Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malengo ya milenia lazima yafikiwe asema Ban Ki-moon

Malengo ya milenia lazima yafikiwe asema Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema bado kuna kazi ngumu ya kuhakikisha malengo ya milenia yanatimizwa.

Akiwakilisha ripoti yake iitwayo ‘Kutimiza ahadi' mbele ya wanachama wa Umoja wa Mataifa amesema ikiwa imesalia miaka mitano tuu kufikia wakati waliojiwekea wa kutimiza malengo ya milenia hapo 2015, bado dunia iko njia panda.

Amesema nchi nyingi zimejitahidi na kupiga hatua za kufikia malengo hayo, lakini bado kuna nchi nyingi ambazo zinasuasua. Ameongeza kuwa changamoto ni kubwa.

Matatizo ya kiuchumi, upungufu wa chakula, mabadiliko ya hali ya hewa na majanga ya asili yote yanatishia juhudi za kufikia malengo hayo, lakini amesema fursa bado ipo kuhakikisha yanafikiwa.