Viongozi wa kimataifa wanaohudhuria COP15 wamo mbioni kuharakisha mapatano kabla ya mwisho wa wiki
Viongozi wa kimataifa, wamo mbioni, wakijaribu kukamilisha mazungumzo ya kuleta itifaki mpya, Ijumaa ijayo, itakayoyasaidia Mataifa Wanachama kudhibiti kihakika, madhara yanayochochewa na hali ya hewa ya kigeugeu.
Mpaka sasa, hatujapata fununu hakika kuhusu utaratibu utakaotumiwa, kuhamisha mabilioni ya misaada ya fedha, kutoka nchi zenye maendeleo ya viwanda, fedha zinazohitajika kutumiwa na mataifa yanayoendelea, ili kuyawezesha mataifa masikini kukabiliana vyema na madhara yanayotokana na uchafuzi wa hali ya hewa isiofuata majira. Kuna mvutano mkubwa baina ya wajumbe wa kutoka nchi tajiri na wale wajumbe wa kutoka nchi masikini, juu ya utaratibu wa kutumiwa kupunguza utoaji wa gesi chafu zinazoharibu mazingira kimataifa.