Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sera lazima zishughulikie hatari za zamani za masuala ya fedha ili kukabili changamoto mpya:IMF

Sera lazima zishughulikie hatari za zamani za masuala ya fedha ili kukabili changamoto mpya:IMF

Shirika la fedha duniani IMF linasema mfumo wa kimataifa wa fedha imeimarika kuliko ilivyokuwa miezi sita iliyopita, lakini bado kuna changamoto kadhaa.

Ripoti mpya ya IMF kuhusu hali ya kifedha duniani inasema watunga sera wasipochukua hatua za kushughulikia matatizo ya awali, mafanikio yaliyopatikana katika masoko ya fedha hayatoendelea na changamoto mpya zitajitokeza.

Ripoti hiyo inaangazia masuala muhimu mawili ya awali ambayo ni chimbuko la mdororo wa kiuchumi na licha ya mafanikio yaliyojitokeza karibuni bado suala la mikopo ni tatizo katika bara Ulaya na pembezoni. Ripoti inasema mambo haya mawili yanatoa cngamoto kubwa katika masuala ya fedha uchumi wa eneo hilo .

Ripoti hiyo pia imebaini kwamba hatari mpya zinahusiana na mfumo na sera za fedha ambazo ziliwekwa ili kukabiliana na mdororo wa kiuchumi. Sera hizo zinawajibu muhimu wa kuchagiza uchumi , lakini zikitumiwa kwa muda mrefu zinawerza kuleta madhara kama kuchukua hatari ya kupindukia, kushindwa kujikwamua na upotevu wa mali.

Nab mwisho ripoti imetoa wito wa kuwa na sera imara ili kupunguza mgawanyiko wa masuala ya fedha barani Ulaya , ili kusaidia kuinua tena masuala ya mikopo na kuboresha tahamani ya sarafu ya Muungano wa Ulaya, lakini pia watunga sera wametakiwa kukabiliana na changamoto mpya, hasa kwa kuzilinda bank zake.