Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jaribio la kuhimili Tsunami eneo la Karibia kufanyika leo

Jaribio la kuhimili Tsunami eneo la Karibia kufanyika leo

Nchi thelathini na tatu duniani leo zitashiriki katika zoezi maalum la tahadhari ya tetemeko la chini ya ardhi, tsunami lenye lengo la kupima utayari wa kukabiliana na janga hilo kwa nchi husika.

Jaraibio hilo ambalo litazihusu nchi za Mashariki mwa Pwani ya Canada, Marekani, Ghuba ya Mexico na Bermuda limeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kupitia tume ya kiserikali ya elimu ya maswala ya bahari.

Kwa mujibu wa mpangilio wa zoezi, tetemeko la ardhi lenye uzito wa 8.5 katika  kipimo cha richa litapiga kilometer 90 katika pwani ya mji wa Oranjestad,cna  Aruba katika bahari ya Karibia kwa muda mmoja.

Zoezi kama hilo limewahi pia kufanyika katika miaka ya 2008 na 2011 katika bahari ya Pasifiki, na mwaka 2009 na 2011 katika bahari ya Hindi. Jumla ya matetemeko ya ardhi 75 yametokea katika eneo la Karibia kwa kipindi cha miaka 500.