Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wataka kutekelezwa kwa haki za binadamu

Umoja wa Mataifa wataka kutekelezwa kwa haki za binadamu

Miaka ishirini baada ya mataifa kukubaliana kuhusu njia za kuboresha haki za binadamu, mpangilio wa kimataifa umewekwa na hatua zimepigwa lakini hata hivyo haujatekelzwa kwenye nchi nyingi kwa mujibu wa maafisa kutoka Umoja wa Mataifa. Jason Nyakundi na taarifa kamili:

(Taarifa ya Jason)

Akiongea kwenye warsha iliyoandaliwa pembeni mwa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataia , mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa katika kile sehemu kuanzia maendeleo na mizozo Umoja wa Mataifa umepungukiwa. Pillay amevitaja vizingiti vya kisiasa kama moja ya sababu kuu inayozuia utekelezwaji akiongeza kuwa nchi ndizo zinajukumu la kutekeleza haki za binadamu. Jitihada za Umoja wa Mataifa zilizo na lengo la kulinda haki za binadamu na maisha wakati wa mizozo mara nyingi hazipati uungwaji mkono wa kisiasa. Pillay ametoa mfano wa Syria ambapo amesema kuwa hali ya haki za binadamu haitaimarika bila ya ushirikiano wa kisiasa katika kuboresha haki za binadamu. Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliason ameunga mkono matamshi hayo akisisitiza kuwa kuna uhusiano kati ya maendeleo , amani na haki za binadamu.