Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Operesheni za kuwarejesha wahamiaji wa Burundi zaihusisha UNHCR

Operesheni za kuwarejesha wahamiaji wa Burundi zaihusisha UNHCR

Mapema wiki hii, Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) Ijumatatu lilishiriki kwenye juhudi za kuwarejesha Burundi wahamiaji 529, kutoka kambi ya Kigeme, iliopo kwenye Wilaya ya Nyammgabe katika Rwanda kusini.

Hili ni fungu la kwanza kati ya wahamiaji 1,495 wanaojiandaa kurudishwa makwao Burundi, kwa ushirikiano miongoni mwa mataifa jirani mawili ya Burundi na Rwanda, ambayo yamedhamiria kuifunga kambi ya Kigeme katika mwisho wa Mei.