Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi ya 50 wauawa kambi ya wakimbizi wa ndani Nigeria:UNHCR

Watu zaidi ya 50 wauawa kambi ya wakimbizi wa ndani Nigeria:UNHCR

Kamishina mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi Filippo Grandi leo Jumatano ameelezea kushtushwa kwake na shambulio la bomu kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Assumpta Massoi na taarifa zaidi

(TAARIFA YA ASSUMPTA)

Grandi amesisitiza haja ya serikali ya Nigeria kuchunguza shambulio hilo lililokatili maisha ya watu zaidi ya 50 na kujeruhi wengine wengi ili kubaini mapungufu yaliyosababisha shambulio hilo.

Duru zinasema miongoni mwa waliopoteza maisha kwenye kambi hiyo ya Rann jimbo la Borno ni wafanyakazi sita wa misaada ya kibinadamu ambapo mauati ilikuwakuta asubuhi ya Jumanne wakiwa katika shughuli za kugawa chakula.Kambi hiyo ilianzishwa Machi 2016 na inahifadhi watu 43,000 waliokimbia nyumba zao miaka miwili iliyopita kuepuka madhila ya Boko Haram.

Grandi amesema hilo ni janga kubwa na wahusika ni lazima wabainike na kuwajibishwa.