Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mashambulizi dhidi ya MSF nchini Yemen

Ban alaani mashambulizi dhidi ya MSF nchini Yemen

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani mashambulizi yaliyofanywa na ndege za kundi lililoongozwa na Saudia dhidi ya kituo cha afya cha Médecins sans Frontières (MSF) mjini Taiz, nchini Yemen.

Taarifa iliyotolewa leo na msemaji wake imesema kwamba watu saba wamejeruhiwa na kituo kimeteketezwa kabisa, kwa mujibu wa MSF.

Katibu Mkuu alikuwa amelaani mashambulizi mengine ya tarehe 27, Oktoba ambapo hospitali ya MSF ilipigwa makombora kwenye jimbo la Sa'ada.

Aidha Bwana Ban amesisitiza kwamba vituo vya afya na wauguzi wanapswa kutunzwa kulingana na sheria ya kibinadamu ya kimataifa, na hivyo ametoa wito ili uchunguzi thabiti utekelezwe juu ya shambulio la leo.

Hatimaye amekumbusha pande za mzozo juu ya wajibu wao wa kuheshimu sheria ya kibinadamu ya kimataifa na haki za binadamu na kujizuia kushambulia raia na miondumbinu ya umma.