Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yazindua ripoti kuhusu vyombo vya habari Palestina

Nembo la UNESCO

UNESCO yazindua ripoti kuhusu vyombo vya habari Palestina

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, limezindua leo ripoti kuhusu vyombo vya habari Palestina katika hafla iliyoandaliwa mjini Ramallah na pia kurushwa moja kwa moja kwa video Gaza.

Ripoti hiyo imetokana na miezi 18 ya utafiti uliofanywa kwa ushirikiano na Kituo cha Maendeleo ya Uandishi habari cha Chuo Kikuu cha Birzeit, na imefuata vigezo vya kimataifa vilivyowekwa na UNESCO, ikiwa ni ya tatu katika ukanda mzima wa nchi za Kiarabu, baada ya zile zilizotolewa Misri na Tunisia.

Ripoti hiyo inatambua kuwepo kwa hakikisho la uhuru wa kujieleza katika sheria ya msingi ya Palestina, ambayo inashikilia nafasi ya katiba, huku ikipendekeza sheria hiyo kuimarishwa. Imependekeza pia kuwa vizuizi vya kisheria vilivyopo katika uhuru wa kujieleza vinapaswa kurekebishwa ili sheria hiyo ishahabiane na viwango vya kimataifa.