Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wananchi wanataka uwajibikaji wa viongozi, na ni haki yao: Dkt. Asha-Rose

UN Photo/Paulo Filgueiras
Dkt. Asha-Rose Migiro, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba Tanzania. (@

Wananchi wanataka uwajibikaji wa viongozi, na ni haki yao: Dkt. Asha-Rose

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limefanya mjadala wa ngazi ya juu kuhusu mchango wa haki za binadamu na utawala wa kisheria kwenye ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015. Miongoni mwa watoa mada alikuwa Dkt. Asha-Rose Migiro Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba wa Tanzania na Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa  Mataifa. Punde baada ya kutoa mada Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa alimuuliza kwa kina suala la haki za binadamu  na hapa Dkt, Asha-Rose anaanza kuelezea ujumbe wake.