Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

16 JULAI 2024

16 JULAI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kutoka hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo Gerald Geofrey Mweli, Katibu Mkuu kutoka wizara ya kilimo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuotoa mkutano wa HLPF amezungumza na Flora Nducha. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.

  1. Muda unazidi kuyoyoma kwa raia wanaokabiliwa na njaa nchini Sudan, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wameonya leo wakati mazungumzo yanayohusisha pande zinazozozana nchini humo yakiendelea mjini Geneva wiki hii.
  2. Dharura ya kibinadamu nchini Haiti inahitaji uangalizi wa haraka, Wawakilishi kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), na Idara ya Ulinzi wa Raia na Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Ulaya (ECHO) wamesema walipokamilisha ziara ya siku nne nchini humo.
  3. Na Cote d'Ivoire ikiwa inakabiliwa na kuongezeka kwa matatizo ya maji na athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye rasilimali za maji inazopakana na majirani zake, nchi hiyo sasa imejiunga na Mkataba wa Maji wa Umoja wa Mataifa wa kuboresha usimamizi wa pamoja wa maji katika mipaka.
  4. Mashinani ikiwa hivi karibuni dunia imetoka kuadhimisha siku ya idadi ya watu duniani shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi UNFPA likisihi mataifa yote duniani kuelimisha uma kuhusu mchango wa sensa katika malengo ya maendeleo endelevu, nampisha kijana kutoka Mwanza, nchini Tanzania akieleza umuhimu wa sensa katika utendaji wa serikali.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
9'59"