Skip to main content

Chuja:

Idadi ya watu

17 MEI 2023

Jaridani hii leo tunaangazia machafuko nchini Sudan na mchakato wa uchaguzi nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Kenya na Mashinani yunasalia hapa makao makuu kusikia ujumbe kuhusu idadi ya watu duniani.

Mwanamke akichuuza chakula katika soko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC
UN Women/Carlos Ngeleka

Ripoti mpya ya UNFPA yabainisha ongezeko la wasiwasi kuhusu idadi ya watu duniani

Data mpya zinaonesha wasiwasi kuhusu ongezeko la idadi ya watu umeenea na serikali duniani zinazidi kupitisha sera zinazolenga kuinua, kupunguza au kudumisha viwango vya uzazi. Lakini juhudi za kushawishi viwango vya uzazi mara nyingi hazifanyi kazi na zinaweza kumomonyoa haki za wanawake, kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu duniani UNFPA kuhusu Hali ya Idadi ya Watu Duniani.  

11 JULAI 2022

Hii leo jaridani tunamulika masuala ya idadi ya watu na amani Sudan Kusini. Katika idadi ya watu ikiwa leo ni siku ya idadi ya watu duniani tunajulishwa kuwa ifikapo tarehe 15 mwezi Novemba mwaka huu idadi ya watu duniani itafikia bilioni 8! Na miongoni mwa nchi ambazo idadi ya watu inaongezeka ni Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Katika masuala ya amani huko Sudan Kusini mafunzo yameendeshwa ili jamii iweze kuwa sehemu ya kukabiliana na ukatili ikiwemo wa kingono. Makala  inakupeleka Mexico kwa msichana  ambaye ndoto yake ya kuwa mkunga ili kusaidia jamii yake imetimia.

Sauti
9'58"