Skip to main content

Chuja:

HLPF

UN Photo/Violaine Martin

Fulgence Kayishema, Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari huenda atahukumiwa nchini Rwanda - Serge Brammertz

Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ofisi ya mwendesha mashtaka ya mfumo wa kimataifa wa kushughulikia mabaki ya kesi za mauaji ya kimbari, IRMCT iliyoko Arusha Tanzania, Serge Brammertz ameeleza kuwa Fulgence Kayishema, mmoja wa watuhumiwa vinara waliokuwa wanasakwa zaidi kwa kuhusika na mauaji ya kimbari nchini Rwanda, aliyekamatwa juzi Mei 24 huko Paarl nchini Afrika Kusini huenda akapelekwa nchini Rwanda kukabiliana na mkono wa sheria kutokana na tuhuma za kushiriki kuwaua watu zaidi ya 2000 wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.

Sauti
4'47"

26 MEI 2023

Jaridani hii leo tunaangazia ripoti kuhusu matumizi ya tumbaku na wakimbizi wa Sudan. Makala tunaangazia mauaji ya kimbari nchini Rwanda na mashinani tutakupeleka nchini Chad, kulikoni?

Sauti
14'21"
UNHCR Video

Mama akiwa na wanae ukimbizini Chad asimulia yaliyomsibu Sudan

Walimuua mume wangu, walijeruhi mwanangu na mimi walinipiga, ni simulizi ya mama ambaye sasa yuko na watoto wake nchini Chad akitokea Sudan kwani nchini mwake ni kama wasemavyo wahenga, Amkani si shwari kufuatia mapigano yaliyoanza tarehe 15 mwezi Aprili mwaka huu ambayo pamoja na kuua zaidi ya watu 700 wengine zaidi ya 300,000 wamekimbilia nchi jirani ikiwemo Chad na miongoni mwao ni Hawaye Ibrahim.

Audio Duration
3'18"
© UNICEF/Shehzad Noorani

WHO: Nchi ziache kutoa ruzuku kwa wakulima wa tumbaku

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limezisihi nchi kuacha kutoa ruzuku kwa wakulima wa tumbaku na badala yake kuelekeza usaidizi wao kwenye mazao endelevu yatakayo wanufaisha mamilioni ya watu.

Katika kuelekea sikuya kupinga matumizi ya tumbaku duniani itakayoadhimishwa Mei 31 WHO inasema  , watu milioni 300 ulimwenguni wanakabiliwa na uhaba wa chakula wakati huo huo zaidi ya hekta milioni 3 katika nchi 120 zinatumika kulima tumbaku, hata katika zile nchi zenye tatizo la njaa.

Sauti
2'30"