Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Unyanyapaa ni changamoto kubwa katika vita dhidi ya COVID-19 Uganda

Suala la unyanyapaa wa aina yoyote ile ni mtihani mkubwa katika jamii kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ambao hutoa wito kila uchao kuhakikisha changamoto hiyo inatokomezwa .Wakati huu wa mlipuko wa janga la virusi vya Corona au COVID-19 unyanyapaa umeelezwa kujitokeza na kusababisha changamoto kwa

Sauti -
6'25"

24 APRILI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo Flora Nducha anakuletea

-Mwezi mtukufu wa Ramadhani unaanza leo kote duniani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa awatakia kila la heri Waislam wote na kusema kwamba COVID-19 itaifanya Ramadhan ya mwaka huu kuwa tofauti kabisa

Sauti -
10'46"

Ushirikiano wa kimataifa wazinduliwa kufanya chanjo na tiba ya COVID-19 kupatikana kwa wote

Mkakati mpya wa kimataifa umezinduliwa leo ili kusongesha mbele juhudi za maendeleo, uzalishaji na fursa sawa ya nyenzo mpya za kukabiliana na janga la virusi vya corona au COVID-19 hasa katika upatikanaji wa chanjo.

 

Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu ni tofauti kabisa- Guterres

Waumini wa dini ya kiislamu ulimwenguni wakianza kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa ujumbe wake wa kuwatakia heri katika mfungo wa sasa ambao amesema ni tofauti kabisa na mingine iliyotangulia kwa ajili ya janga la COVID-19.

Kwa kila siku inayopita, athari za janga la COVID-19 na matokeo yake ni dhahiri :UNFPA

  Kwa kila siku inayopita, athariza janga la COVID-19 na matokeo yake ni dhahiri :UNFPA

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA , limesema linashikamana na wale wote wanaojitolea na kuwa katika mstari wa mbele kupigana na janga la virusi vya corona au COVID-19: kuanzia kwa wahudumu wa afya na wanaojitolea kusaidia bila malipo.