Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Katibu Mkuu Antonio Guterres akipanda meli ya Kubrosliy huko Odesa, Ukraine.
UN Photo/Mark Garten

Kila meli inayoondoka Odesa imebeba matumaini- Guterres

Leo hii Odesa ni zaidi ya bandari ya kusafirisha, shehena, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo alipotembelea bandari hiyo iliyoko Ukraine, kujionea upakiaji wa shehena za nafaka na chakula kufuatia makubaliano ya kusafirisha nafaka kupitia Bahari Nyeusi, makubaliano yaliyowezesha kuanza kusafirishwa kwa bidhaa hizo kwenda soko la dunia licha ya uvamizi unaoendelea wa Urusi nchini Ukraine.