Nuru ya matumaini ya amani ya kudumu yaanza kuchomoza Sudan- UN
Ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja tangu mapinduzi ya kijeshi nchini Sudan, vyama vya siasa vimeanza mazungumzo mwezi huu yenye lengo la kurejesha kipindi cha mpito kinachoongozwa na raia, hatua ambayo Umoja wa Mataifa imepongeza ikisema ni muhimu katika kufikia amani na demkrasia.