Tunachukua hatua lakini ukatili wa kingono bado umeota mizizi- Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wakati sasa umewadia kuchukua hatua mpya ili kutokomeza ukatili wa kingono kwenye mizozo, wakati huu ambapo vimeshamiri kuanzia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Sudan Kusini hadi Myanmar.