Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

15 Mei 2020

Hii leo Ijumaa kama kawaida ni mada kwa kina na tunammulika muuguzi mkunga kutoka hospitali ya Kairuki nchini Tanzania akiangazia ni kwa vipi wanatekeleza majukumu yao ipasavyo katikati ya janga la virusi vya Corona au COVID-19. Muuguzi mkunga huyo amezungumza na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha  Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es salaam. Tutajifunza neno la wiki na mtaalamu Onni Sigalla anachambua neno Kiruka Njia. Habari  kwa ufupi nazo zimo tukiangazia ndege ya kwanza ya abiria kutua Tanzania kupambana na COVID-19.

Audio Duration
10'31"
Pichani iliyopigwa kutoka angani inaonyesha sehemu ya makazi kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya
Picha/Siegfried Modola

Nimeongeza uzalishaji sabuni, nikapunguza bei, ili kupambana na COVID-19-Havyarimana

Ili kusaidia kupambana na kusambaa kwa virusi vya corona, mkimbizi kutoka Burundi, Innocent Havyarimana anayeishi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya na ambaye kwa miaka mitano amekuwa akijihusisha na utengenezaji wa sabuni za maji, hivi sasa ameongeza uzalishaji na kupunguza bei ya sabuni ili watu wengi waweze kunawa mikono yao.

Sauti
2'25"