Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Guterres:Tukihakikisha haki za wenye ulemavu, tunawekeza katika mustakbali wa Pamoja
Katika mazingira ya kawaida watu wenye ulemavu mara nyingi hukosa fursa ya huduma za msingi kama vile elimu, huduma za afya na fursa za kiuchumi au ushiriki katika jamii.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika uzinduzi wa sera kuhusu watu wenye ulemavu na janga la corona au COVID-19.
Katika uzinduzi huo Bwana Guteres amesema janga la COVID 19 linaathiri kila nyanja ya jamii zetu na leo hii anaelezea jinsi gani janga hili linavyoathiri watu bilioni moja wenye ulemavu duniani.
06 Mei 2020
Leo katika Jarida la Umoja wa Mataifa tunaangazia habari tofauti kutoka sehemu mbalimbali duniani:
-Tutasikia kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu uzinduzi wa sere za watu wenye ulemavu na janga la corona au COVID-19.
-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linashirikiana na jamii ili kusaidia kuepusha kusambaa kwa ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 hususan kwenye maeneo ya makazi duni huko Kenya.
UNICEF Kenya yaungana na wafanyakazi wa kujitolea kutokomeza Corona
Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linashirikiana na jamii ili kusaidia kuepusha kusambaa kwa ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 hususan kwenye maeneo ya makazi duni
Tukihakikisha haki za wenye ulemavu, tunawekeza katika mustakbali wa Pamoja:Guterres
Katika mazingira ya kawaida watu wenye ulemavu mara nyingi hukosa fursa ya huduma za msingi kama vile elimu, huduma za afya na fursa za kiuchumi au ushiriki katika jamii.