Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Utalinda vipi watoto dhidi ya Corona?
Ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 ukitangazwa kuwa ni janga la dunia kwa kuwa umesambaa duniani kote, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wametangaza mwongozo mpya wa kusaidia kulinda watoto na shule dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo.
Sasa virusi vya Corona vina dalili ya kuenea duniani kote- WHO
Hatimaye ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 umetangazwa kuwa sasa una dalili ya kuenea duniani kote, amesema Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya ulimwenguni, WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus akizungumza na wanahabari mjini Geneva, Uswisi hii leo.
Idadi ya wanaoingia jengo la UN New York yapunguzwa kwa asilimia 60 ili kupambana na COVID-19
Wakati maambukizi mapya ya virusi vya Corona au COVID-19 yakiendelea kuongezeka katika nchi nyingi duniani na idadi ya waliofariki kutokana na virusi hivyo ikiongezeka kila uchao, Umoja wa Mataifa nao umechukua hatua kudhibiti maambukizi kwa kupunguza idadi ya wafanyakazi wanaofika kazini kila siku kwa asilimia 60. Hii ni kwa kuzingatia kuwa tayari visa vimeripotiwa katika miji kadhaa ikiwemo New York, Marekani ambako ndiko makao makuu ya chombo hicho.
11 Machi 2020
UN yachukua hatua madhubiti kudhibiti COVID 19. Mataifa lazima yafundishe watoto wa kiasili na wale wa jamii za wachache kwa lugha yao wenyewe asema mtaalam wa UN. Usiache mila na deturi zikazima ndoto zako ashauri Mama mwendesha Bodaboda Palagie Gerald.
COVID-19: Idadi ya wanaoingia jengo la UN New York yapunguzwa kwa asilimia 60 wakiwemo wafanyakazi