Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

06 MACHI 2024

06 MACHI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia mizozo na janga la kibinadamu nchini Sudan, na kuondoka kwa MONUSCO nchini DRC.  Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Uganda, kulikoni? 

  1. Takriban miezi 11 tangu majenerali wapinzani watangaze vita nchini Sudan, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa leo walionya kwamba mzozo huo unaweza kusababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani.
  2. Harakati za ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, za kuondoka nchini humo zikiendelea, tunamulika hatua chanya zilizochukuliwa na ujumbe huo katika kunusuru vijana waliokuwa wanatumikishwa na waasi mashariki mwa nchi hiyo. 
  3. Katika makala na tukielekea Siku ya Wanawake Duniani ambayo mwaka huu ina maudhui “Wekeza kwa wanawake: Harakisha maendeleo,”, tunatembelea wajasiriamali Kajiado nchini Kenya kusiki ni kwa jinsi gani wanawezakujiumudu kiuchumi.
  4. Na mashinani tunaelekea nchini Uganda kumsikia mkimbizi kutoka nchini Sudan Kusini.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
12'4"