Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

16 FEBRUARI 2024

16 FEBRUARI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa usalama unaofanyika mjini Munich Ujerumani, na elimu kwa watoto katika mzozo nchini Afghanistan. Makala tunasikia ujumbe kuhusu matatizo kwa upande wa taaluma ya utangazaji wa redio. Mashinani tunasikia ujumbe wa mkulima nchini Kenya.

  1. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo katika mkutano wa usalama unaofanyika mjini Munich Ujerumani ametoa wito wa kuwepo utaratibu wa kimataifa ambao unafanya kazi kwa kila mtu.
  2. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF linafanya kila juhudi kuhakikisha watoto wanapata mahitaji yao ikiwemo elimu. Huko nchini Afghanistan shirika hilo limehakikisha zaidi ya wanafunzi 683,000 wanapata elimu wangali katika mazingira wanayoishi. 
  3. Katika makala na ikiwa wiki hii ulimwengu umeadhimisha Siku ya redio Duniani, Mwanahabari gwiji wa siku nyingi nchini Tanzania Rose Haji anakubaliana na mtazamo wa Umoja wa Mataifa kuwa redio bado ni chombo muhimu sana katika mawasiliano ya ulimwengu lakini anaona kwamba kwa upande wa taaluma ya utangazaji wa redio kuna tatizo.
  4. Mashinani tunakuletea ujumbe wa Agnes, mwanamke mkulima kutoka Kenya ambaye alikuwa anategemea chakula cha msaada kutoka Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP lakini leo, kupitia mtaro wake wa maji inayopeleka maji kwa shamba lake, anavuna mazao yake ya kutosha familia yake na ameweza kujimudu kimaisha kwa kuuza masalio.

Mwenyeji wako ni Evarist Mapesa, karibu!

Audio Credit
Evarist Mapesa
Sauti
10'42"