Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

26 JANUARI 2024

26 JANUARI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia maamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ vitendo vya mauaji ya kimbari katika mashambulizi ya Israel dhidi ya wapalestina huko Gaza. Pia tunamulika viwanda vya nishati safi ulimwenguni, makala ikitupeleka nchini India. Mashinani tnakuletea ujumbe wa mhamiaji ambaye ni mchezaji wa musiki, mwalimu na rafiki nchini Burundi.

  1. Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ hii leo imeamua kuwa Israel lazima ichukue hatua zote za kuzuia vitendo vya mauaji ya kimbari katika mashambulizi yake dhidi ya wapalestina huko, Gaza, uamuzi unaofuatia shauri lililowasilishwa na Afrika Kusini la kutaka Mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa ichukue hatua za awali kwa mujibu wa Mkataba wa kimataifa wa kuepusha mauaji ya kimbari wa mwaka 1948. Assumpta Massoi amefuatilia na kuandaa taarifa ifuatayo.     
  2. Kilimo ni moja ya shughuli za kibinadamu zinazochangia katika uchafuzi wa hewa. Kwa kulitambua hilo, FAO kote ulimwenguni inachagiza kile inachokiita kwa lugha ya kiingereza Bioeconomy yaani uchumi ambao msingi wake unatokana na matumizi ya rasilimali za kibayolojia zinazopatikana kwenye mazingira; kwa mfano kurejesha taka katika uzalishaji wa nishati safi, mbadala wa mafuta ya kisukuku. Kupitia harakati hizo, FAO inasaidia wakulima kuongeza mapato, kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi na kuchangia kupunguza taka ulimwenguni kwa kubadilisha mifumo ya zamani ya kilimo ambayo ilikuwa inachangia kuharibu mazingira.
  3. Na makala ikiwa leo ni maadhimisho ya kwanza kabisa ya siku ya kimataifa ya nishati safi nakupeleka Tanzania kuangazia juhudi zinazofanyika kuhamasisha umma kuhamia kwenye nishati safi au jadidifu kutimiza lengo namba 7 la maendeleo endelevu SDGs. Vijana wako msitari wa mbele katika harakati hizo na miongoni mwao ni Nuzulack Dausen mwanzilishi wa Jukwaa la kidijitali la Jiko point linaloendesha kipindi cha mwanaume jikoni kupitia mtandao wa Youtube. Amezungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Stella Vuzo afisa habari wa Umoja wa Mataifa na kumfafanulia wanavyochangia katika kufanikisha lengo la maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa      kuhusu nishati safi . 
  4. Mashinani tutaelekea katika Jiji la Bujumbura nchini Burundi kumsikia mhamiaji ambaye ni mchezaji wa musiki, mwalimu na rafiki.      

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'7"