Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

30 OKTOBA 2023

30 OKTOBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika eneo linalokaliwa na wapaestina Gaza. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Ethiopia, kulikoni?

  1. Huku mzozo wa Israel na Palestina ukiwa katika wiki yake ya nne, wahudumu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa leo wameonya kuhusu shinikizo      linaloongezeka kwenye hospitali za kaskazini mwa Gaza ambako wamesalia wagonjwa na wahudumu wa afya, huku kukiwa na ripoti za kuongezeka kwa  operesheni za ardhini za jeshi la Israel. 
  2. Wakati mzozo katika Ukanda wa Gaza ukizidi kuongezeka huku wananchi wakikabiliwa na changamoto nyingine lukuki ikiwemo uhaba wa chakula, maji, mafuta na vifaa vya matibabu vya kuokoa maisha, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu na Afya ya Uzazi UNFPA limesema mfumo wa afya nao uko ukingoni kuanguka. Shirika hilo limezungumza na wanawake wajawazito walioko Gaza kuhusu hali mbaya wanayokabiliana nayo. 
  3. Katika makala Evarist Mapesa anakupeleka nchini Kenya ambapo mabadiliko tabianchi umesababisha kupotea kwa upatikanaji wa elimu, huduma muhimu, na ajira kwa vijana nchini Kenya, Hata hivyo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini humo kwa kushirikiana na Equal Access International wanawawezesha vijana kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko tabianchi na kutoa ufahamu kuhusu suluhisho la kukabiliana na tatizo hilo.
  4. mashinani na tutaelekea nchini Ethiopia, kushuhudia jinsi gani Umoja wa Mataifa unavyasaidia watoto kuondokana na utapiamlo uliokithiri. 

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
13'18"