Mashariki ya Kati

Wapalestina wasubiri hadi lini kupata suluhu yenye haki?-Mahmoud Abbas

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amehoji kwa viongozi wa dunia kwenye mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 75 unaoendelea leo Ijumaa mjini New York Marekani na kwa kupitia mtandao kuwa watu wake wanapaswa kusubiri mpaka lini ili kuweza kupata suluhu yenye haki? .

Umoja wa Mataifa wakaribisha maendeleo kuelekea uundaji wa eneo lisilo na silaha za nyuklia, Mashariki ya Kati

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amekaribisha kufanikiwa kwa Mkutano wa Uanzishwaji wa eneo huru la silaha za nyuklia na silaha zingine za maangamizi mkubwa katika Mashariki ya Kati, uliofanyika wiki hii katika Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York.

 

Mchango wa wanahabari katika amani ni mkubwa:UN

Wandishi wa habari ni wadau muhimu katika mchakato wa kurejesha amani katika ukanda wa Mashariki ya Kati ambako mzozo umesambaratisha uchumi na harakati za kibinadamu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataiaf,

Sauti -
1'29"

Mchakato umekwama Mashariki ya Kati, ghasia zashamiri, amani mashakani- Mladenov

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye mchakato wa amani Mashariki ya Kati, Nickolay Mladenov ameonya kuwa hatua za haraka zinahitajika ili kurejesha mchakato wa amani kwenye eneo hilo kwa mujibu wa maazimio ya Umoja wa Mataifa huku akitoa wito kwa viongozi wa pande zote za Israel na Palestina kuchukulia hatua makundi yenye misimamo mikali.

Mgawanyiko Mashariki ya Kati ni mkubwa lakini kuna fursa ya kutatua- UN

Eneo la Mashariki ya Kati lina mgawanyiko mkubwa lakini ndaniya changamoto hizo kuna fursa hatimaye mustakabali wenye nuru kwa wakazi wa eneo hilo.

Njaa yaendelea kuizogoma Afrika ya Kaskazini na Mashariki ya Kati:FAO

Tatizo la njaa linaendelea kuongezeka katika ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini (NENA) ambako watu milioni 52 wanakabiliwa na lishe duni na utapiamlio , imesema leo ripoti ya shirika la chakula na kilimo FAO.

Vita dhidi ya ugaidi yashika kasi mashinani

Kila uchao, magaidi wa kitaifa na kimataifa wanaibuka na mbinu mpya, vivyo hivyo tunapaswa kusaka mbinu mpya za kukabili vitendo hivyo viovu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Sauti -
1'56"

Ghasia Gaza; vituo vya afya vyazidiwa uwezo

Wahudumu wa afya huko Gaza, Mashariki ya Kati hivi sasa wanahaha kutibu zaidi ya majeruhi 2700 wa ghasia za jana zilizosababisha vifo vya watu zaidi ya 58. Taarifa zaidi an Assumpta Massoi.

Zahma ya leo Mashariki ya Kati ina athari kwa dunia nzima:Mladenov

Hali ya Mashariki ya Kati ni tete, na inahitaji mshikamano wa pamoja kuhakikishasuluhu inapatikana na amani ya kudumu inadumishwa ili kuepusha zahma kwa dunia nzima , sasa na hata baadaye.

Nina hofu na maandamano yaliyopangwa Ijumaa Gaza: Mladenov

Mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati, Nickolay Mladenov, amesema anafuatilia kwa hofu kubwa maandalizi ya maandamano makubwa ya marejeo yaliyopangwa kufanyika Kesho Ijumaa Ukanda wa Gaza.