wajawazito

Ubunifu wa UNICEF Malawi kusambaza chanjo ya Covid-19 mtaa kwa mtaa wazaa matunda

Mnyumbuliko wa hivi karibuni wa virusi vya Corona vinavyosababisha Covid-19, Omicron ukiwa umesambaa ulimwenguni kote, ukosefu wa usawa wa chanjo unaweka baadhi ya watu hatarini zaidi kuruhusu minyumbuliko kubadilika na kuathiri wanadamu wengine. Afrika ina idadi ya chini zaidi ya watu waliochanjwa dhidi ya COVID-19 duniani lakini nchini Malawi mradi bunifu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa kusambaza chanjo kwa njia ya gari unaongeza upatikanaji wa chanjo na imani ya chanjo miongoni mwa wanawake wajawazito katika jamii za vijijini.

17 Juni 2021

Katika Jarida hii leo utasikia kuhusu Ujumbe wa Katibu Mkuu wa UN kuhusu kulinda Mazingira,  WHO yaonya ongezeko la wajawazito wanojifungua kwa njia ya Upasua

Sauti -
12'45"

Watoto milioni 116 kuzaliwa miezi 9 baada ya COVID-19 kutangazwa janga, je changamoto ni zipi?

Kuelekea siku ya mama duniani tarehe 10 mwezi huu wa Oktoba, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linakadiria kuwa watoto milioni 116 watakuwa wamezaliwa wiki 40 tangu ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 utangazwe kuwa janga la kimataifa tarehe 11 mwezi Machi mwaka huu.

Sasa wajawazito na watoto wanapata tiba ya malaria kuliko wakati mwingine wowote:WHO

Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la afya ulimwenguni WHO, inaonyesha kwamba wanawake wajawazito na watoto wanapata tiba zaidi ya malaria hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote ingawa juhudi na ufadhili vinahitajika kuchochea zaidi hatua za kimataifa dhidi ya ugonjwa huo.

Kebehi, matusi, makaripio vyakumba wajawazito wakati wa kujifungua, unasema utafiti wa WHO

Utafiti mpya wa Shirika la afya ulimwenguni, WHO, unaonesha kwamba theluthi moja ya wanawake katika nchini 4 za kipato cha chini wameripoti kukumbwa na mateso

Sauti -
1'39"

09 Oktoba 2019

Hii leo habari yetu kubwa ni kuhusu utafiti uliofichua jinsi wanawake wanavyokumbwa na mateso wanapokuwa wanajifungua, makaripio, kukemewa na kadha wa kadha. Kisha ni harakati za kukabili mlipuko wa surua huko DR Congo, ugonjwa ambao sasa ni tishio kuliko hata Ebola.

Sauti -
10'54"

Kebehi, matusi, makaripio vyakumba wajawazito wakati wa kujifungua- Utafiti

Utafiti mpya wa Shirika la afya ulimwenguni, WHO, unaonesha kwamba theluthi moja ya wanawake katika nchini 4 za kipato cha chini wameripoti kukumbwa na mateso wakati wa kujifungua.

08 Agosti 2019

Hii leo Assumpta Massoi anaanzia  na ripoti mpya yenye lengo la kudhibiti ongezeko la joto duniani, watu wanashauriwa kupunguza kula nyama, kulikoni, kisha anakwenda Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC ambako ujumbe wa serikali ya taifa hilo na ujumbe kutoka Rwanda wamekuwa na mazungumzo juu ya

Sauti -
11'1"

14 Juni 2019

Hii leo Ijumaa ni mada kwa kina ikimulika mtoto wa kike nchini Tanzania mwenye umri wa miaka 16 ambaye amebuni apu ya kukumbusha wanawake wajawazito kuhusu ujauzito wao na kwenda kliniki.  Ubunifu wenye tija kwenye mazingira yake.

Sauti -
10'33"