HABARI KWA UFUPI
Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 umefungua pazia rasmi mjini Dubai katika Falme za nchi za Kiarabu kwa kuwaleta Pamoja wajumbe zaidi ya 60,000 kuangalia jinsi ya kuongeza hatua, fursa ya nyenzo za kujenga mnepo ikiwemo makubaliano ya kuanzishwa mfuko wa hasara na uharibifu ambayo yamepitishwa kwenye mkutano huo na pia kutumia ubunifu kudhibiti janga hilo.
Guterres aonya kwamba kifanyikacho Antarctica sasa hakisalii tena huko kinasambaa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko ziarani katika eneo la ncha ya kusini mwa dunia, Antarctica amesema eneo hilo limekuwa likijulikana kama eneo lenye manufaa makubwa lakini lililosahaulika, lakini sasa limeamshwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi.
24 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia amani na usalama katika ukanda wa Gaza na msaada wa kibinadamu nchini Chad. Makala tunakupeleka nchini Tanzania, na mashinani tunamulika Ibara ya 13 ya Tamko la Haki za Binadamu.
Nigeria: Maadhimisho ya Siku ya Watoto Duniani yaangazia athari za mabadiliko ya tabianchi kwa watoto
Ikiwa leo ni siku ya mtoto duniani, nchini Nigeria wametumia siku hii kutathmini athari wanazozipata watoto kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Katika taifa hilo lililopo Afrika Magharibi lenye jumla ya watu milioni 233 watoto wanachukua asilimia 51 ya taifa hilo ndio maana mashirika ya Umoja wa Mataifa , serikali na wadau wengine wakaona haja ya kutumia siku hii kuzungumza namna bora ya kuwasaidia.
Mataifa lazima yaende mbali zaidi kuliko ahadi za sasa kutokomeza uzalishaji wa Hewa Chafuzi - UNEP
Wakati joto la ulimwengu na uzalishaji wa hewa chafuzi vikivunja rekodi katika mwaka huu wa 2023, Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) ya Pengo la Uzalishaji hewa chafuzi iliyotolewa leo Novemba 20 mjini Nairobi Kenya imeeleza kwamba imegundua kuwa ahadi za sasa chini ya Mkataba wa Paris zinaweka ulimwengu kwenye mstari wa ongezeko la joto la nyuzi joto 2.5 hadi 2.9 za Selsiasi zaidi ya viwango vya kabla ya kuanza kwa viwanda katika karne hii.
Ripoti: Mtoto 1 kati ya 3 anakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji - UNICEF
Mtoto mmoja kati ya Watoto watatu au sawa na watoto milioni 739 duniani kote - tayari wanaishi katika maeneo yaliyo na uhaba mkubwa au wa juu sana wa maji, na mabadiliko ya tabianchi yanatishia kufanya hali hii kuwa mbaya zaidi, imebainisha ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Jumatatu kwa saa za New York, Marekani.
Wenyeji Baringo nchini Kenya wanufaika kufuatia mradi wa maji wa WFP
Uhakika wa upatikanaji wa maji ni moja ya suluhisho za kupambana na mabadiliko ya tabianchi hususan katika maeneo yanayokabiliwa na ukame. Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP kwakushirikiana na serikali wamewezesha wananchi wa kaunti ya Baringo kuondokana na adha ya maji.