Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

10 MEI 2023

10 MEI 2023

Pakua

Jaridani hii leo tunaangazia machafuko nchini Sudan na hali ya wakimbizi wa ndani na wale wanaosaka hifadhi katika nchi jirani. Makala tunaangazia afya ya uzazi na watoto wanaozaliwa njiti  na mashinani tunakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?

  1. Takriban watu milioni 2 hadi milioni 2.5 wanatarajiwa kutumbukia kwenye janga la njaa nchini Sudan katika miezi michache ijayo kwa sababu ya vita inayoendelea nchini humo limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP.
  2. Nchini Chad, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeanza kazi ya kusajili wakimbizi walioingia nchini humo kutoka Sudan kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa RSF kwenye mji mkuu wa taifa hilo Khartoum. Wakimbizi sasa pamoja na kusajiliwa wanapatiwa mahitaji muhimu.
  3. Makala tunaangazia Ripoti mpya iliyotolewa hii leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) na la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na PMNCH ambao ni Ushirikiano wa mkubwa zaidi unaoangazia Afya ya Mama, watoto na vijana kuhusu Kuzaliwa kabla ya wakati inazitaja sababu kama vile mimba za utotoni na shinikizo kubwa la damu wakati wa ujauzito (pre-eclampsia), kuhusika kwa karibu na watoto kuzaliwa njiti.
  4. Mashinani tutakupeleka nchini Tanzania ambapo mwanaharakati wa wasichana anatoa ujumbe kuhusu changamoto ambazo wasichana wanazipitia.

Mwenyeji wako ni Assumta Massoi, Karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'30"