Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

01 SEPTEMBA 2022

01 SEPTEMBA 2022

Pakua

Katika Jarida la mada kwa kina hii leo Flora Nducha anakuletea

-Msimu mpya wa shule ukianza sehemu mbalimbali duniani , takwimu mpya zilizotolewa leo mjini Paris Ufaransa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO zinaonyesha kwamba watoto na vijana milioni 244 wenye umri wa kati ya miaka 6 na 18 duniani kote bado hawako shule.

-Mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths leo ameanza ziara nchini Somalia kushuhudia hali halisi ya njaa na kutathimini mahitaji ya walioathirika na ukame na hatua zinazochukuliwa kuwasaidia.

-FAO leo limekaribisha mchango wad ola milioni 83 kutoka kwa serikali ya Marekani wenye lengo la kupiga jeki shirika hilo katika operesheni zake za dharura na kujenga mnepo nchini Ethiopia, Afghanistan na Sudan, lakini pia maeneo mengine ya Haiti, Jamhuri ya Dominika, Burkina Faso, Sahel na ukanda wa Afrika Magharibi.

-Mada kwa kina inatupeleka Mwanza Tanzania kumulika maabara za sayansi zinazotembea kwa lengo la kusaidia na kuchagiza wanafunzi kusoma masomo ya sayansi

-Na katika kujifunza Kiswahili leo tunaelekea Zanzibar katika baraza la Kiswahili BAKITA kumulika methali isemayo "Maneno mengi si huja"

Audio Credit
UN News/Flora Nducha