Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

12 JANUARI 2021

12 JANUARI 2021

Pakua

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa Flora Nducha anakuletea

-Mashirika manne ya kimataifa ya afya na misaada ya kibinadamu yametangaza kuanzishwa kwa hifadhi ya chanjo ya Ebola ulimwenguni ili kuhakikisha upatikanaji wa chanjo kwa haraka pindi panapotokea mlipuko wa ugonjwa huo hatari.

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema watoto hawawezi kumudu mwaka mwingine wa kuvurugwa kwa masomo yao likitoa wito wa kila juhudi kufanyika kuhakikisha shule zinafunguliwa hata wakati wa COVID-19

-Mradi wa lishe wa AFIKEPO unaoendesha na UNICEF, FAO kwa ufadhili wa  Muungano wa Ulaya  EU waimarisha afya za watoto nchini Malawi 

-Makala leo inatupeleka Uganda kumulika ushiriki na hamasa ya wanawake katika uchaguzi mkuu wa Uganda utakaofanyika keshokutwa Januari 14

-Na mashinani tunasalia Uganda eneo la Kitgumu ambako utamsikia mama mjane aliyesaka msaada wa kisheria kupata haki yake na kuepuka dhuluma baada ya mumewe kufariki dunia

Audio Credit
UN News/ Flora Nducha
Audio Duration
12'7"