Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

03 JANUARI 2020

03 JANUARI 2020

Pakua

Miongoni mwa Habari anazokuletea Flora Nducha katika Jarika letu la kina Ijumaa hii ni pamoja na 

-Wakimbizi 500   kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wameingia Uganda kufuatia mapigano mapya siku ya mwaka mpya limesema shirika la wakimbizi UNHCR

-Nchini Libya waroketi yameanguka karibu na kituo cha wakimbizi na wasaka hifadhi na kuleta hofu kubwa ya usalama wa watu hao

-Sudan Kusini shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM limesema mtoto wa miaka minne aliyetekwa Oktoba 28 mwaka 2018 baada ya mama yake aliyekuwa mfanyakazi wa IOM kuuawa ameachiliwa huru na kuunganishwa na baba yake mzazi mjini Juba.

-Mada yetu kwa kina leo inamulika mchango wa chama cha waandishi wa habari wanawake visiwani Zanzibar nchini Tanzania TAMWA katika kumkomboa mwanamke

-Na katika kujifunza Kiswahili juma hili mchambuzi wetu Onni Sigalla kutoka Baraza la Kiswahili la Kitaifa BAKITA anaelezea matumuzi na maana ya neno "KUJIZATITI"

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Audio Duration
9'58"