Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwiano wa kijografia na usawa wa kijinsia ni muhimu katika vita dhidi ya ugaidi:

Uwiano wa kijografia na usawa wa kijinsia ni muhimu katika vita dhidi ya ugaidi:

Pakua

[caption id="attachment_326649" align="aligncenter" width="623"]overnightboronkov

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye ni mkuu wa ofisi mpya iliyoanzishwa kwenye Umoja huo kupambana na ugaidi anaamini kwamba uwiano wa kijiografia na usawa wa kijinsia ni chachu ya mafanikio ya ofisi yake.

Vladimir Voronkov aliteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres mwezi juni , baada ya baraza kuu kuidhinisha kuanzishwa kwa kwa ofisi mpya kusaidia nchi wanachama kutekeleza mkakati wa kimataifa wa kupambana na ugaidi.

Ofisi hiyo ikiwa na wafanyakazi 30 kutoka nchi 25 na asilimia 70 wakiwa ni wanawake, bwana Voronkov anasema mustakhbali wake unatia matumaini.

(VORONKOV CUT)

"Nadhani kitu cha muhimu ni kuwa na kitengo kinachohusisha nchi nyingi na suala hili la uwiano wa kijiografia ni muhimu sana katika uwezekano wa kuboresha masuala mengi, suala la pili muhimu ninalotaka kutaja ni kwamba tuna uswa mzuri wa kijinsia katika ofisi hii kwa sababu asilimia 70 ni wanawake , suala la jinsia na usawa wa kijinsia ni moja ya chachu kubwa ya kuhakikisha mafanikio ya kitengo hiki.”

Photo Credit