Skip to main content

ILO yaunda mkakati wa kuinua vijana wajasiriamali

ILO yaunda mkakati wa kuinua vijana wajasiriamali

Pakua

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya wajasiriamali wa kati na wadogowadogo, mashirika ya Umoja wa Mataifa yamezindua mkakati wa kimataifa wa kuhakikisha kazi bora kwa vijana ili kuinua ajira kwa kundi hilo.

Makakati huo unasimamiwa na shirika la kazi ulimwenguni ILO, ambalo limesema kuwa ni jukwaa mahususi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya ajira na kusaidia nchi wanachama katika kutimiza lengo la ajira bora kama ilivyoanishwa kwenye malengo ya maendeleo endelevu SDGs namba nane.

ILO inasema kwamba mkakati huo utaanikizwa na kampeni ya kupigia chepuo wajasiriamali vijana kufanikiwa na kuimarisha fursa za ajira binafsi kwa vijana.

Katika kutimiza hilo, kuanzia mwezi Juni hadi Agosti, kampeni hiyo itajikita katika kumulika vikwazo dhidi ya vijana kuingia katika ulimwengu wa wajasiriamali, ikiwamo ukosefu wa sera na mazingira toshelevu, ukosefu wa mitaji na vifaa vya kuimarisha ujuzi na maarifa.

ILO inashirikiana na kituo cha kimataifa cha biashara ITC, shirika la Umoja wa Mataifa la mfuko wa mitaji UNCDF, Kamati ya Umoja wa Mataifa ya baishara bna maendeleo UNCTAD na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda UNIDO.

Photo Credit
Wajasiriamali wadodo wadogo wachangia uchumi. Picha; ILO